Wimbo wa nne kutoka kwenye EP yake mpya ya nyimbo 7, chini ya KhanMusic. Ngoma hii mpya inaitwa “Merijaah”, na inasimulia mapenzi ya karibu – ujirani uliozaa mahaba ya kweli.
Kwa sauti yake tamu na utunzi wa kipekee, Mbooso anatupeleka kwenye simulizi la mpenzi aliyeanza kama jirani wa kawaida, lakini penzi likazaliwa na kujaa taratibu mpaka kufika hatua ya dhati kabisa:
“Jirani yangu jirani yangu, tumezoeana,
Mlango wake, mlango wangu – zinatazamana…”
Na kilichofuata ni wazi:
“Mwishowe tukapendana – oooh meri merijaaah,
Kama ingekuwa ndoo ya maji ingejaa,
Na kama ingekuwa nguo mwilini ningevaa…”
Mapenzi Ya Ukaribu – Yaliyojaa Hisia
“Merijaah” ni wimbo laini wenye mdundo wa kupapasa moyo, na mistari ya kutia tabasamu. Mbooso amefanikisha kuonyesha uzuri wa mapenzi ya kawaida yaliyojaa ukaribu, ucheshi na ukomavu. Ni aina ya wimbo unaokufanya utafakari kuhusu yule jirani ambaye moyo wako ulianza kumpenda polepole tu.
Download “Merijaah” – Mbooso (MP3)
📥 Pakua wimbo mpya wa Mbooso “Merijaah” hapa: